Zifuatazo ni baadhi ya nukta muhimu zilizokuja katika Khutba yake: 1_ Maelekezo ya kimaadili katika Qur’an, yakiwemo uaminifu, uvumilivu, heshima kwa wengine, na haki katika matendo. 2_Umuhimu wa kutekeleza maadili mema katika maisha ya kila siku badala ya kuyajua kwa nadharia tu.

24 Oktoba 2025 - 20:02

Jamiatul Mustafa (s) - Malawi | Sheikh Abdul_Rasheed Shuaib Azungumzia Maadili Katika Qur’an Tukufu Katika Sala ya Ijumaa +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Kituo cha Kidini cha Al-Mustafa nchini Malawi, idadi kubwa ya waumini na wafuasi wa mafundisho ya Kiislamu walihudhuria. Msemaji wa tukio, Sheikh Abdulrasheed Shuaib, alijadili mada ya “Maadili katika Qur’ani Tukufu.”

Sheikh Shuaib alisisitiza umuhimu wa maadili mema katika maisha ya mtu binafsi na jamii ya Waislamu, akibainisha kuwa Qur’ani ni mwongozo kamili kwa mwanadamu kufikia fadhailo na tabia njema. Alieleza kwamba maadili ya Kiislamu hayalengwi tu kuridhisha Mwenyezi Mungu, bali pia kuunda jamii yenye afya, mshikamano na amani.

Baadhi ya hoja na nukta kuu za hotuba yake ni:

1_Maelekezo ya kimaadili katika Qur’an, yakiwemo uaminifu, uvumilivu, heshima kwa wengine, na haki katika matendo.

2_Umuhimu wa kutekeleza maadili mema katika maisha ya kila siku badala ya kuyajua kwa nadharia tu.

3_Athari za maadili mema katika kuimarisha umoja na mshikamano wa jamii ya Waislamu.

4_Nafasi ya viongozi na walimu wa dini katika kuelimisha na kueneza maadili mema kwa vijana.

Sala ya Ijumaa iliendelea kwa furaha na shauku, huku hotuba ya Sheikh Shuaib ikipokelewa kwa mikono miwili na washiriki. Mwisho wa hotuba, Sheikh aliwahimiza waumini kuzingatia mafundisho ya maadili mema ya Qur’ani katika maisha yao na kuwa mfano wa vitendo vya maadili mema ya Kiislamu.

Your Comment

You are replying to: .
captcha